August 27, 2026 12:22 pm
"Where Africa Comes to Stay Informed."
US Edition
Breaking
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
  • Storm system strengthens off the coast, evacuation orders expand
  • Parliament passes landmark energy bill after overnight session
  • Tech index rebounds after early sell-off on chip earnings
  • Peace talks resume in Geneva as envoys return to the table
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
Home / Entertainment / Meta Yafuta Akaunti Milioni 3.7 Kukomesha Udanganyifu Afrika Magharibi
Entertainment Meta Yafuta Akaunti Milioni 3.7 Kukomesha Udanganyifu Afrika Magharibi

Meta Yafuta Akaunti Milioni 3.7 Kukomesha Udanganyifu Afrika Magharibi

Meta imesema imeondoa zaidi ya akaunti, kurasa na vikundi milioni 3.7 kutoka Facebook na Instagram, kama sehemu ya operesheni ya pamoja iliyolenga mitandao ya udanganyifu inayofanya kazi katika eneo la Afrika Magharibi.

Operesheni Kubwa ya Kimataifa

Katika taarifa iliyotolewa mtandaoni Jumanne, kampuni hiyo ilisema operesheni hiyo ilihusisha makampuni mengine 14 ya teknolojia pamoja na vyombo vya dola kutoka nchi 10, hatua iliyowezesha kubainika kwa zaidi ya vituo 30 vinavyoshukiwa kuendesha udanganyifu.

Operesheni hiyo iliratibiwa na Shirika la Kupambana na Uhalifu la Uingereza (National Crime Agency), likishirikiana na Idara ya Sheria ya Marekani, Shirika la Upelelezi la Shirikisho (FBI) na vyombo vingine vya dola.

Waokolewa Ghana

Kwa mujibu wa Meta, vyombo vya dola vilithibitisha kukamatwa kwa watu 28 na kuokolewa kwa watu 117 waliokuwa wamesafirishwa kinyume cha sheria na kulazimishwa kufanya kazi katika vituo vya udanganyifu nchini Ghana.

Kampuni hiyo ilisema waathirika waliookolewa walikuwa wamezuiliwa kinyume cha ridhaa yao katika jengo la makazi, mahali walikokumbwa na utapiamlo pamoja na unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia.

Walengwa Hasa Marekani na Uingereza

Meta iliongeza kuwa akaunti nyingi zilizoondolewa, ikiwemo kurasa na vikundi, zililenga watu wanaoishi Marekani na Uingereza kupitia wasifu bandia uliojifanya kuwa wa raia wa Marekani na Uingereza.

Microsoft nayo ilisimamisha akaunti zinazoshukiwa kuhusika na matukio hayo ya udanganyifu.

Makampuni Mengine Yanayoshiriki

Wakati huohuo, kampuni ya fedha za kidijitali (cryptocurrency) ya Coinbase ilisema ilibaini zaidi ya waathirika 65 wa udanganyifu waliokuwa bado hai kwenye mfumo, na kuzuia hasara iliyokadiriwa kuzidi dola za Marekani 415,000.

Makampuni mengine yaliyoshiriki ni pamoja na Google, OpenAI, Starlink na Adobe, pamoja na vyombo vya dola kutoka Nigeria, Ghana, Australia, Canada, New Zealand na India.

Aina za Udanganyifu Uliolengwa

Operesheni hiyo ililenga udanganyifu wa uwekezaji wa fedha za kidijitali, matangazo bandia ya ajira, udanganyifu wa kimapenzi, kujifanya maafisa wa usalama au majeshi, mauzo bandia mtandaoni, pamoja na mbinu za kuwalenga tena waathirika wa awali kwa kuwaahidi kurejesha fedha walizopoteza endapo watalipa kiasi fulani mapema.

Kauli ya Meta

Makamu wa Rais na Naibu Mshauri Mkuu wa Sheria wa Meta, Chris Sonderby, alisema operesheni hiyo imeonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya makampuni ya teknolojia na vyombo vya dola, akiongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na washirika wake kukomesha mitandao ya udanganyifu.

Entertainment
0 0

Comments

0
No comments yet. Be the first to share your thoughts.
Lang
Powered by Google
Customer Support

Hello! 👋 Welcome to Zone Yetu customer support. How can we assist you today?

Now
Powered by AI • Average response time: <1s